Thursday, November 1, 2012

SABABU YA KUSITISHA KUWEKA HABARI NA MATUKIO

TUNAOMBA RADHI KWA KUTOENDELEA  KUWEKA HABARI NA MATUKIO KWENYE BLOG YETU.HII NI KWASABABU TUNABADILIKA KUTOKA KWENYE BLOG KWENDA KWENYE TOVUTI.TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO WENU.

Saturday, October 20, 2012

ANTI EZEKIEL AFUNGA NDOA ABADILI DINI SASA ANAITWA RAHMA



   Baada ya siku chache kutangaza katika vyombo vya habari kwamba anatarajia kuolewa sasa habari imekamilika. Ezekiel amefunga ndoa jana mida ya saa mbili za usiku baada ya kubadili dini na kujulikana kama Rahma kuanzia hivi sasa na mchumba wake anaejulikana kwa a.k.a  Demonte  na baada ya kufunga ndoa hiyo aliamua kuweka ushahidi huu katika mitandano mbalimbali kwamba mashabiki wake wote pamoja na marafiki wafahamu kwamba ameshaolewa. TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA MAISHA YAKO YA NDOA

Saturday, October 13, 2012

MNYAMA ‘TID’ KUJA NA ALBAMU ALIYOIPA JINA LA ‘KIUNO’, AONGELEA UJIO WA ‘TV SHOW’ PIA…!!


MSANII mkongwe ndani ya game la mziki TID, au unaweza kumuita sauti ya pesa, amesema kuwa baada ya ngoma yake ya ‘Kiuno’ kufanya vizuri sasa anatarajia kuachia albamu ambayo itakuwa na nyimbo nane huku kukiwa na kazi nyingine ambazo hakuwahi kuziachia.

Hata hivyo alisema kuwa jina la albamu hiyo imebebwa na goma yake ya ‘Kiuno’, ambapo ngoma nyingine zitakavyokuwepo ndani ni pamoja na ‘Raha’, ‘Check Me’, na nyingine kibao kwani alishindwa kutaja majina kwa madai kuwa wasanii wa sasa wana tabia ya kuiba majina na kuyafanyia kazi.

Aliongeza kuwa albamu imeshakamilika na kitu kinachosubiriwa sasa ni uzinduzi kwani, anaamini ujio huu utamfanya aweze kurudi kwenye chati kama ilivyokuwa zamani.

Hata hivyo aliongeza kuwa suala lake la ‘TV Show’, anayotarajia iruke hewani ni kwamba walitarajia kuanza hivi karibuni lakini wamerudi nyuma kidogo kwani bado wapo mezani na wadhamini wake ili waweze kufikia muafaka mzuri wa kufanya kazi ambayo itakuwa na manufaa pande zote.

DIAMOND AWA NA FURAHA BAADA YA KUTAJWA KUWA KING OF BONGO FLAVA NA MTANDAO WA MSN


Siku ya juzi mtandao mkubwa Duniani kwa jina la MSN uliweza kutangaza majina mawili ya wasanii wa Tanzania kama ndio bora zaidi kwa kuwapa vyeocha King na Queen of Bongo flava.Wasanii hao waliotajwa na kupewa vyeo ni mtu mzima Diamond Platinum wa wasafi na mwanadada Lady J Dee baada ya kupata taarifa hii kutoka katika mtandao mkubwa duniani unaojulikana kwa jina la MSN sasa bhana Diamond akaamua kuandika ujumbe katika site yake baada ya kutajwa katika mtandano huo
"Honestly nmejiskia furaha sana kuandikwa katika mtandao mkubwa kama huu,
juu ya kazi yangu ya muziki ninayoifanya na kupewa heshima ya kuwa King of Bongo Flava.
Hii inaonesha ni jinsi gani muziki wetu umepiga hatua na unazidi kuvuka boda" Huu ndiyo ujumbe uliyoandikwa na mtu mzima Platinum baada ya kutaja katika mtandano mkubwa Duniani unaojulikana kwa jina la MSN.

VURUGU JIJINI DAR HAPATOSHI




  ENEO la Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam jana liligeuka uwanja wa mapambano kati ya makundi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Waislamu na polisi baada ya watu hao kuvamia Kituo cha Polisi Kidogo cha Maturubai kilichopo eneo hilo.
Watu hao walivamia kituo hicho wakitaka wakabidhiwe mtoto anayedaiwa kukojolea kitabu kitakatifu cha Quran ili wamwadhibu.
Vurugu hizo zilizoanza tangu saa nne asubuhi, zilisababisha makanisa matano kuchomwa moto, magari kadhaa kuvunjwa vioo na watu hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime alisema watu kadhaa wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo... “Siwezi kutaja idadi ya waliokamatwa, lakini kuna watu tunawashikilia kutokana na kufanya fujo, kwa sasa niko katika operesheni, nitazungumza kwa kirefu baadaye.”
Hata hivyo, Misime alisema hakuna kifo kilichotokea wala majeruhi.
“Pamoja na kwamba bado tupo katika eneo la tukio bado hatujashuhudia vifo wala majeruhi na tunaomba Mungu mambo hayo yasitokee.
Aliyataja makanisa hayo kuwa ni la TAG Kizuiani, Wasabato Kizuiani, TAG la Shimo la Mchanga na KKKT Mbagala Zakheim.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchomaji wa makanisa hayo ni kosa la jinai na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu hao.
Alisema katika vurugu hizo gari la Mkuu wa Polisi Wilaya ya Temeke (OCD) limevunjwa vioo.
Kamanda Kova alisema Jeshi hilo litaimarisha ulinzi katika makanisa hayo ili kuhakikisha kunakuwa na usalama.
Miongoni mwa magari hayo matano yaliyoharibiwa katika vurugu hizo ambazo zilisababisha Barabara ya Kilwa kufungwa kwa muda ni gari la Kituo cha Televisheni cha Clouds ambalo lilivunjwa vyoo.
Akizungumzia suala hilo, mkazi wa Mbagala Mission, Nassor Mohamed alisema vurugu hizo zilitokea baada ya mtoto mmoja kukojolea Quran.
Alisema mtoto huyo alifikia hatua hiyo baada ya kuwapo na ubishi na mtoto mwenzake ambaye wanasoma wote katika Shule ya Sekondari Chamazi.
Mohamed alisema mtoto huyo mwenye miaka 14, alikuwa akibishana na mwenzake mwenye umri kama huo kwamba mtu akikojolea kitabu hicho hugeuka kuwa nyoka.
Alisema kuwa mtoto huyo aliamua kufanya kitendo hicho ili kuona kama atageuka nyoka na wakati akifanya kitendo hicho mzee mmoja alimuona na kumhoji kisha kumpeleka kwa mama yake na kumshtaki.
“Yule mama aliwajibu kuwa kama ni hilo tu, basi awape hela wakanunue kingine. Aliposema hivyo wale watu wakakasirika wakamwambia, sisi tulikuja kukuambia kwa uzuri ili umwadhibu mwanao, lakini kutokana na majibu yako hatukuachii tena huyu mtoto,” alisema.
Alisema baada hapo, watu hao walimpeleka mtoto huyo katika Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Chamazi ambako waliandikiwa barua na kumpeleka kituo kidogo cha polisi kilichopo katika eneo hilo.
Jumatano jioni, watu hao walifika katika kituo hicho wakitaka wapewe tena mtoto huyo na ndipo walipoambiwa kuwa amehamishiwa katika Kituo cha Maturubai.
Alisema baada ya kumkosa mtoto huyo walihamasishana na kukubaliana kuwa baada ya kutoka msikitini kesho yake (jana), wakavamie kituo hicho na kumtoa mtoto huyo.
Wakati ghasia hizo zikiendelea, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Temeke, Farid Salehe aliwasihi waumini wa dini hiyo kuwa watulivu.
Katibu wa Vijana wa Bakwata Mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkarim Kulao aliwataka Waislamu waliokuwa wamekusanyika katika eneo la kituo hicho cha polisi kurejea majumbani kwao kwani mtuhumiwa huyo alikuwa ameshahamishwa.
Baadaye Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanyisha baadhi ya watu waliokuwa wamekiendelea kubaki katika eneo hilo.
Askari waliokuwa na mabomu ya machozi walitawala eneo hilo kuweka ulinzi na hatimaye kufanikiwa kuwatawanya watu hao.
Baada ya kutimuliwa katika mkusanyiko huo, kundi moja la watu hao lilifika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mbagala na kulichoma moto.
Mzee wa Kanisa hilo, Siaga Kiboko alisema mali kadhaa zimeharibika na kwamba walishatoa taarifa polisi.