Mama wa mtoto mmoja anayeitwa Blue Ivy
na mke wa mkali wa Hip Hop duniani Legend The man himself Jay – Z,
Beyonce wikendi hii ataperform ikiwa ni show ya kwanza kwa takribani
zaidi ya mwaka sasa alikuwa hajaperform kutokana na kubanwa au kupata
muda wa kutosha kumlea mtoto wake Blue Ivy. Concert hiyo itakuwa huko
katika jiji la Atlantic siku ambayo itakuwa ni siku ya kukumbukwa.
Wakati wa mazoezi (rehearsal) kwa
ajili ya concert hiyo Beyonce alionekana bado ni noma alikwenda na beat
fresh wimbo wa “Halo” na akajifunza mitindo mipya wakati wa rehearsal
hiyo. Beyonce alianza rehearsal mwezi mmoja uliopita “ Da nouma aisee,
naifikiria hii concert sana, nanafuraha kubwa kuwa mama, lakini sasa
narudi kazini, itakuwa ngeni kidogo, ni muhimu kwamba hupotei bado
unakipenda unachokipenda, nimerudi, nimerudi kazini” Alifunguka Beyonce.

No comments:
Post a Comment