![]() Mtoto aipojifungua mtoto mwenzake |
Alitakiwa
kwa wakati huu awe anacheza na watoto wenzake lakini msichana mmoja wa
nchini Kolombia mwenye umri wa miaka 10 ameanza ulezi wa mtoto wake wa
kike baada ya kujifungua salama mtoto wa kike mwenye afya njema,
kichekesho ni kwamba amegoma kumnyonyesha mwanae.
|
|
| Msichana
mmoja wa nchini Kolombia jina lake limehifadhiwa, amekuwa miongoni mwa
wasichana wenye umri mdogo duniani kujifungua mtoto. Msichana huyo toka kabila la watu wanaopenda kuishi maporini la Wayuu la jimbo la La Guajira lililopo kaskazini mwa Kolombia, alijifungua mtoto baada ya mimba yake kutimiza wiki 39. Aliwasili hopitali akivuja damu akilia kutokana na uchungu wa kujifungua. Madaktari walifanikiwa kumzalisha kwa njia ya upasuaji kwa kuhofia umri wake mdogo. Mama huyo mwenye umri mdogo na mtoto wake mwenye uzito wa kilo 2.27 wote wanaendelea vizuri kwenye hospitali waliyolazwa na madaktari wameongeza kuwa mtoto wa msichana huyo ana afya njema. Kituko kilichotokea ni kwamba mama huyo mwenye umri wa miaka 10 amegoma kata kata kumnyonyesha mtoto wake huyo. Polisi wa nchini Kolombia wamedai kuwa wanaweza kumchukulia hatua mwanaume aliyempa ujauzito msichana huyo mdogo ingawa pia sheria za Kolombia huwa zina upendeleo maalumu kwa kabila la Wayuu kuwasaidia wadumishe mila zao ambapo si jambo geni kuona wasichana kupata ujauzito wakiwa na umri mdogo. Kesi ya mtoto huyu imekuwa gumzo nchini Kolombia huku jina la baba wa mtoto huyo likiwa halijajulikana ingawa magazeti ya Kolombia yamekuwa yakitofautiana katika taarifa zao baadhi yakidai mwanaume aliyempa mimba binti huyo ana umri wa miaka 15 huku magazeti mengine yakidai ni mwanaume mwenye umri wa miaka 30. | ||
Thursday, May 10, 2012
MADHARA YA WASICHANA KUDANGANYIKA.......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment