Matokeo ya kidato cha sita yametangazwa jana huku shule za binafsi zikiibnuka vinara katika matokeo hayo.Shule za binafsi zimefanya vibaya na sababu ziko wazi,mazingira ya kusomea katika shule za serikali ni mabovu mno.
Shule za serikali hazina walimu wa kutosha,miundombinu mibovu,hazina maabara na kadhalika.Haya yote yanawanyima wanafunzi fursa ya kusoma kwa matumaini ya kufaulu mitihani yao.Hivi kweli katika hali kama hii tutegemee ufaulu wa miujiza?.
Serikali haina budi kuitazama sekta ya elimu kwa jicho pevu kwani kumekuwa na ongezeko la wimbi la vijana wengi mitaani wanaoishi katika mazingira hatarishi kwani hawana shughuli maalumu za kufanya baada ya kushindwa kuendelea na masomo.
Kwa mliofaulu hongereni sana na kwa mliofanya vibaya,huu sio mwisho wa maisha!!!!
No comments:
Post a Comment