Friday, June 22, 2012

HUU NDIO MKOKO WA DIAMOND, KITU MILLION 60


 



Staa wa muziki wa kizazi kipya  Bongo, Naseeb Abdul  ‘Diamond  Platinumz’ amevuta mkoko wa Kijanja  wenye thamani ya ‘mkwanja wa Kibongo Milioni  60 keshi.


Akizungumza muda mfupi  baada ya  kupokea  ‘dinga’ hiyo aina ya Land Cruiser Prado TX  kutoka kwa wakala aliyekuwa akishughulikiwa  mpango mzima  wa  kuingia kwake  hapa  Bongo, Diamond  alifunguka kuwa alikuwa na mpango wa kuvuta  mkoko ‘dizaini’ hiyo kitambo lakini  kuna mambo kadhaa yakawa  yanachelewesha.




“Nashukuru Mungu kuwa mpango wangu umetimia, nilipanga hivi kitambo lakini kuna baadhi ya mambo yalichelewesha hatua hiyo, najua watu watasenama mengi kuhusu hili lakini ukweli ni kuwa huu ni mchuma wangu” alisema Diamond.



Katika hatua nyingine Diamond alifunguka kuwa awali alinunua mdinga kama hiyo huko visiwani Zanzibar, lakini baada ya kuikagua aligundua kuwa lina matatizo na kuamua kulirudisha na kuagiza kitu kipyaaaaaa

No comments:

Post a Comment