Friday, September 14, 2012

MJENGO WA EPIQ BSS ni noma

                          MJENGO ambao wataishi washiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012, umeleta mzuka kwa baadhi ya washiriki ambao wameazimia kujifua kuhakikisha wanatimba kula bata.Wakipiga stori na Showbiz kwa nyakati tofauti, baadhi ya washiriki hao kutoka mikoa mbalimbali walisema jumba hilo limewapa ari na nguvu mpya kufanya mazoezi ya kutosha kuhahakisha wanaingia na kudumu ndani ya mjengo huo kabla ya kung’ara kitaani.
Jengo hilo lilianikwa hivi karibuni licha ya kwamba haikufahamika liko maeneo gani na kwa nje linaonekana ni la kifahari kiasi cha baadhi ya watu kudai kuwa, mandhari ya ndani yanaweza kuwa kama ya lile la Big Brother.

No comments:

Post a Comment