Leo tunatupia macho kwenye shule ya msingi Korotambe huko Tarime ambapo kuna ripoti za kushutua kwamba mwalimu mmoja shuleni hapo anawadhalilisha wanafunzi wa kike kwa kuwafunua sketi zao na kuangalia kama wamevaa "Underskirt" ili kama hawana apate kuwauzia kwani yeye ni mfanyabiashara wa nguo hizo.Katika hali ya kushangaza mwalimu huyo anayeitwa Eliza amekiri kufanya kitendo hicho huku akijinadi kuwa amekua akifanya biashara hiyo kwa muda mrefu sasa.Kitendo hiki kina madhara kisaikolojia kwa wanafunzi ambao wengine husita kwenda shuleni kwa kumhofia mwalimu huyo hivyo kuathiri mustakabali wao kimasomo.Kiukweli ipo haja ya vyombo husika kufuatilia utendaji wa walimu mashuleni na kuhakikisha kuwa shughuli zinazoendeshwa shuleni ni za kimasomo na si vinginevyo.Wanafunzi pia mnao wajibu wa kuwashirikisha wanajamii masuala ambayo mnayahofia ili muweze kupata msaada.Mbali na kuwepo vitendo ya udhaliishaji shuleni hapo,shule hiyo ipo katika hali mbaya na hatarishi kwa wanafunzi kwani miundombinu yake ni chakavu mno hivyo inwanyima wanafunzi fursa ya mazingira mazuri ya kusomea.Nani wa kumlaumu endapo wanafunzi hawa hawatafanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho?
TAFAKARI......
No comments:
Post a Comment