Zijue baadhi ya sababu na madhra ya utumiaji wa madawa ya kulevya
Ukosefu wa ajira
Nchini Tanzania kiwango cha ukosefu wa ajira kimo juu sana.Ukosefu wa ajira
umesababisha vijana wengi kukaa ovyo bila chochote cha kufanya na kugeukia madawa
ya kulevya.
Shinikizo kutokana na
marafiki.
Hii ni moja ya sababu kuu ya kutumia madawa ya kulevya. Wengi wanaotumia
madawa ya kulevya katika ukanda huu wamekubali kwamba walianza kutumia madawa
kwa sababu wengi marafiki wao walikuwa wanatumia .Wengi wa vijana ambao
wanapatikana maeneo ya baharini wanatumia madawa haya ili wapate ujasiri wa
kuzungumza na wateja wao.
Athari:
Uhalifu
Nchini Tanzania, vijana wengi hawawezi kukaa bila kutumia dawa hizi. Dawa
hizi huwa ghali mno na la kusikitisha ni kuwa vijana hawa hawana ajira. Hiii
inamaanisha kuwa vile wanavyoweza kupata pesa ni kwa kuwaibia wakazi wenzao. Hii
inasababisha hali ya usalama nchini kutoaminika.
Maradhi
Hii ni athari kubwa ya madawa ya kulevya. Kuna maradhi mengi ambayo vijana
hawa wanapata kutokana na madawa haya. Baadhi yao wamekuwa wendawazimu.
Maradhi haya yanawapata vijana kwa kasi mno kwa sababu ya kutokula
vyema.Hawa vijana hawali lakini wanaendelea kutumia madawa haya.Pia
wanaambukizana maradhi kwa kubadilishana sindano. Hii imesababisha kuzidi kusambaa kwa
UKIMWI nchini.
Kifo
Mwishowe athari hizi zote zaelekeza kaburini. Kiwango cha vifo Tanzania kinaongezeka kwa kasi mno. Vijana wengi nchini wanaaga dunia
katika miaka yao ya thelathini.Vifo hivi vinasababishwa hasa na maradhi
yanayoletwa na madawa ya kulevya. Hili ni jambo linatia nchi ya Tanzania wasiwasi
kwani vijana wengi ambao ni nguvukazi ya taifa wanaaga dunia.
No comments:
Post a Comment