Sunday, April 29, 2012

COMFIRMED


Tafiti za karibuni zilizofanyika hapa nchini Tanzania zimebaini kuwa vijana balehe wanaanza kutumia dawa za kulevya au vilevi kama sigara na pombe katika umri mdogo. Na wakati huo huo vijana wanakuwa bado hawana elimu ya msingi kuhusu madhara na hatari zitokanazo na utumiaji wa vitu hivyo. Ukosefu wa elimu hii huwaweka vijana hatarini i na hivyo kwenye matatizo ya kiafya, maradhi pamoja maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI na ya kijamii .Habari hii imetayarishwa  ili i kuziba pengo hili la ukosefuwa elimu juu ya dawa za kulevya. Ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa muhimu zilizo sahihi juu ya dawa za kulevya na athari zake kwa vijana na kuwaongoza waweze kukwepa vishawishi vinavyochangia utumiaji wa dawa za kulevya na pia kuwawezesha kuwajibika na kufanya uamuzi mwafaka kwa ajili ya maisha yao. Watu wengi wanafikiri kwamba elimu juu ngono hasa katika umri mdogo inahimiza tabia ya kutowajibika. Lakini kinyume cha haya ndio ukweli halisi. Bila elimu ya kutosha vijana balehe hawawezi kuwajibika kufanya maamuzi sahihi. Uzoefu umeonyesha kwamba vijana wakipewa taarifa wanafanya uamuzi salama.

Dawa za kulevya ni nini?
Tunaposema dawa za kulevya ina maana ni matumizi mabaya ya dawa na hasa pale yatumikapo kinyume cha maelekezo ya tabibu na hivyo kuleta madhara kwa mtumiaji.
Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?
Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika kisheria. Tanzania, dawa za kulevya zinazokubalika kisheria ni pamoja na tumbaku na pombe, pia dawa zilizothibitishwa kwa maandishi na daktari. Dawa zinazotolewa kwa udhibitisho wa madaktari ni zile dawa za kutibu. Pale zinapotolewa kwa sababu nyingine mbali na matibabu au maelezo ya daktari zinakuwa dawa za kulevya. Miongoni mwa dawa zinazotumika vibaya hapa Tanzania ni valium, asprin na panado. Vimiminika kama petroli pia hutumiwa kama dawa za kulevya. Vitu hivi hutumiwa kwa njia ya kuvuta hewa yake kwa pua au mdomo.
Pia kuna vileo visivyoruhusiwa ambavyo hutengenezwa kienyeji kama vile gongo. Dawa za kulevya ambazo hutumika sana Tanzania ni pamoja na bangi, mirungi, mandrax, heroini na kokaini. Kokaini ambayo hupatikana katika hali ya ungaunga ulio mweupe, hutumiwa kwa njia ya kuvuta kwa pua au kuchanganywa na maji na baadaye kujidunga mwilini kwa kutumia sindano. Heroini pia hupatikana kama unga mweupe. Unaweza kuvuta heroini kama sigara au kuvuta hewa yake kwa ndani na pia kwa kujidunga sindano. Katika hali i i isiyo ya kawaida heroini vilevile inaweza kupatikana katika vipande vidogovidogo vya kahawia vijulikanavyo kama “sukari ya kahawia”.
Njia nyingine ya kuzungumzia dawa za kulevya ni kutokana na madhara yake. Yapo madawa ambayo hupagawisha au yanayozubaisha au kupoozesha kama vile kileo, nikotini, dawa za usingizi, kwa mfano valium na heroini. Dawa hizo zinamfanyamtumiaji kujisikia shwari, lakini pia huhuzunisha. Dawa zinazochamngamsha ni  kama mirungi, kokaini na zile za kuvuta, kwa mfano petroli, zina madhara ya kukufanya uhamasike na kujisikia kuwa na nguvu. Dawa zinazopagawisha zinaleta hisia, sauti, taswira, harufu kwa mtu japokuwa vyote hivyo havipo kweli. Bangi ni mojawapo ya dawa hizi.
 Dawa za kulevya zinatoka wapi na zinafika vipi Tanzania?
Dawa za kulevya zinatoka nchi mbalimbali duniani, na baadhi zinatoka hapahapa Tanzania. Mfano kokaini inatoka Amerika ya Kusini, heroini hutoka Bara la Asia, nchi za India, Pakistan na Burma. Dawa zinazotengenezwa viwandani kama mandrax zinatoka nchi nyingi duniani, ikiwemo Tanzania. Bangi na mirungi hulimwa Tanzania. Dawa zilizothibitishwa na madaktari, pamoja na vimiminika vinavyogeuka hewa, kama petroli, zinatengenezwa hapahapa Tanzania.
 VIJANA TUACHANE NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI ZINAATHIRI MUSTAKABALI WA MAISHA.......

No comments:

Post a Comment