Sunday, April 22, 2012

PIGA VITA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Unyanyasaji wa kijinsia ni nini?

Unyanyasaji wa kijinsia ni tendo lolote lenye mtazamo wa jinsia linaloweza kumsababishia mtu adha au kero,madhara na mateso ya kimwili,kisaikolojia na kingono .

Unynyasaji wa kijinsia unasababisha watoto wengi hasa watoto wa kike kuozwa wakiwa wadogo,kupata mimba zisizotarajiwa na kusumbuliwa na madhara na maradhi ya afya ya uzazi na maambukizi ya VVU

Mfano wa unyanyasaji wa kijinsia

Unyanyasaji wa kimwili:Kumpiga,kumfinya,kumpiga mateke,kumtishia mtu wa jinsia tofauti na silaha.
Unyanyasaji wa kisaikolojia:Kumdhalilisha,kumtishia kumwacha na kumnyima mahitaji mtu anayekutegemea.
Unyanyasaji wa kingono:kubaka,ngono na watoto wadogo,kumshikashika mtu kimapenzi bila ridhaa yake.

Njia za kuzuia unyanyasaji wa kijinsia

-Tambua matendo ya unyanyasaji wa kijinsia,na kwamba matendo haya hayakubaliki na ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
-Usikubali kujihusisha katika matendo ambayo hutaki.
-Elimisha rafiki zako kuhusu unyanyasaji wa kijinsia.
-Badili matumizi ya lugha inayowadharau na kuwadhalilisha wanawake.
-Msikilize mwenzi anaposema hayuko tayari kufanya kitu fulani.

Faida za kuzuia unynyasaji wa kijinsia
-Unappunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU.
-Unachangia kuleta mazingira yanayojali usawa na haki kati ya wanaume na wanawake.

                                              PAMOJA TUNAWEZA

No comments:

Post a Comment