Thursday, April 19, 2012

SWAGA ZA WAMASAI KUTOGA MASIKIO ZAWADATISHA WAZUNGU........!!!!!!

KAMA utahadithiwa tu bila kuoneshwa picha halisi za wazungu kutoka Bara la Ulaya ambao wamefika Tanzania na kuvutiwa na mila za Wamasai ya kutoga masikio na wao kuiga, usingeweza kuamini.
Amini usiamini, baadhi ya Wazungu sasa wamewehuka na mtindo huo wa kutoga masikio na wao kutoga kisha kuweka mapambo mbalimbali katika masikio yao.
Inasemekana Wazungu hao baadhi yao walikwenda hadi katika vijiji vya Wamasai mkoani Arusha na kuomba kutobolewa masikio yao na hivi sasa wamekuwa wakiweka mapambo kama wafanyavyo Wamasai.
Wazungu wengine wamekuwa wakiweka hereni zilizotengenezwa kwa shanga, wengine kushindilia masikioni mwao mapambo ya miti ambayo walinunua kwa Wamasai waliowatembelea sehemu za Ngorongoro Crater, kaskazini mwa Tanzania, wengine wanaweka makopo ya vinywaji masikioni na kutoboa pua.

No comments:

Post a Comment