DENTI IFM ASAKWA NA POLISI KWA WIZI
Na Haruni Sanchawa
MSOMI mmoja aliyetajwa kwa jina la Neema Msangi anasakwa na polisi baada ya kudaiwa kumuibia vitu vyote vya ndani na fedha, Restatus Swai anayedaiwa kuwa alikuwa rafiki yake.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinasema kuwa binti huyo anayedaiwa ni mkazi wa Tabata, Dar es Salaam, ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar es Salaam alifanya kitendo hicho hivi karibuni.
Akizungumza na mwandishi wetu, Swai ambaye ni mkazi wa Kinondoni alisema kuwa Neema alikuwa ni rafiki yake na alimuamini.
“Tatizo kubwa ni kwamba si mwaminifu, akiwa anaumwa mimi ndiye nilikuwa ninafanya huduma zote , siku moja, aliniambia kuwa atanikomesha hii ni baada ya kupunguza huduma kwake kutokana na tabia zake,”alisema Swai.
Akifafanua zaidi kijana huyo alidai, kutokana na jinsi alivyomzoea alimjulisha wapi anaacha funguo za nyumba lakini siku moja akaja na kuzoa kila kitu ndani, hivyo kudhihirisha kauli yake ya kumkomesha.
“Nilikwenda kuripoti suala hili la wizi polisi na kesi hiyo imepewa jalada lenye kumbukumbu namba KMJ/RB/487/2012 WIZI na nimewaambia askari Neema ameiba vitu na fedha, wanamsaka,” alisema.
Gazeti hili lilimtafuta Neema na kumuuliza kama kweli amechukua vitu vya mpenzi wake huyo ambapo alikiri.
“Kwanza atambue bado nitamkomesha kama amekimbilia kwa waandishi wa habari, kama ni vitu anavyosema nimechukua mimi sirudishi hata kitu kimoja, aendelea kufanya atakavyo, atanitambua,” alifoka dada huyo.
Alidai baada ya hapo msichana huyo amekuwa akimtumia ujumbe wa kumtisha maisha.
Habari kutoja gazeti la uwazi.

No comments:
Post a Comment