JARIDA
maarufu la Times nchini Uganda limemtaja mama wa watoto wawili Zari
Hassan kuwa ndiye mwanamke mrembo na tajiri kuliko wote nchini humo kwa
wakati huu.
Kwa mujibu wa jarida hilo Zari (30) ambaye ni
Mwanamuziki,Mfanyabiashara na Mtangazaji wa runinga amepata mafanikio
makubwa kwenye muziki na pia kipindi chake cha runinga
kinachofananishwa na kipindi cha ‘Keeping up with the Kardashians’
kinachoendeshwa na mrimbwende wa kimarekani Kim Kardashian.
Huku likiambatanisha picha za magari na nyumba anazomiliki
mwanadada huyo, jarida hilo limeandika kuwa huenda akaingia kwenye
orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika baada ya kipindi kifupi kijacho
endapo ataendelea na mwenendo wake wa sasa kibiashara.
hata hivyo jarida hilo pia limetaja zari kuwa mmoja wa mstaa
wapenda starehe na amekuwa akitumia mkwanja alionao kumnasa mwanaume
wa aina yoyote anahisi kuwa anahitaji kumliza kwa wakati huo ingwa
tuhuma hizo hazikusibitishwa moja kwa moja.
katika
hatua nyingine jarida hilo limesema kuwa Zari mwenye maskani yake pia
nchini Afrika ya Kusini, wazazi wake si raia wa uganda kuzaliwa
ispokuwa ni wahamiji kwani baba yake ni raia wa Buurundi mwenye asili
ya Somalia na mama yake ni raia wa India kutoka kabila la Mutoroo.
Aidha Times limeandika kuwa
Zari anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama BMW –
2006, Black Chrysler – 2008, – Audi Q7 2010 Silver Crysler – 2008,
JETTA-2006, Mercedes Benz convertible -2008. Range-Rover, Lamborghin,
Hummer na mengine mengi huku pia akiwanaumiliki wa maduka, hotel na
majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria, Cape Town na Kampala.




No comments:
Post a Comment