HUYU NDIO MWANAFUNZI WA MIAKA 15 ALIEFUTWA SHULE BAADA YA KUPEWA UJAUZITO.
Mwanafunzi Honolina Msigala aliyefutwa kuendelea na masomo ya elimu ya Msingi baada ya kupata mimba ,kulia ni baba mzazi mzee Msigala na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Isakalilo kulia
MWANAFUNZI Honolina Msigala (15) mkazi wa Isakalilo katika Manispaa ya Iringa aliyekuwa akisoma katika shule ya Msingi Njiapanda katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa amefutwa katika orodha ya wanafunzi wa darasa la saba wanaosubiri kufanya mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya Msingi baada ya kudanganywa kwa Chipsi na soda ya kujazwa mimba na dereva wa lori mjini Iringa aitwae Ndanga Kilovele.
na hiyo imetokea baada ya kuonekana mjamzito na jitihada za mhusika wa mimba hiyo kutaka kuitoa kushindikana.
Uongozi wa shule hiyo ya Msingi Njiapanda umelifuta jina la mwanafunzi huyo katika orodha ya wanafunzi wa shule hiyo kama njia ya kuficha aibu hiyo ya mimba shuleni hapo.
Auzebio Msigala ambae ni baba mzazi wa huyo mtoto amesema mwanae alikuwa akiishi na mama yake mzazi ambae alikuwa akimtumikisha katika shughuli za kuuza pombe jambo ambalo lilimwezesha kijana huyo kutumia mwanya huo kumrubuni mwanafunzi huyo na kuanza mahusiano ya kimapenzi hadi kumpa ujauzito.
Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Prosper Chokala alikiri kuwepo kwa maagizo ya kamati ya shule hiyo ya kumfuta mwanafunzi huyo baada ya kushindwa kuhudhuria vipindi kwa kipindi cha miezi takribani mitano sasa ambapo Mkuu wa shule amekanusha madai ya kupokea shilingi milioni 1 kutoka kwa mtuhumiwa wa huo ujauzito ili kugawana na mzazi kwa ajili ya kumtorosha mwanafunzi huyo
TUKUMBUKE KUMPA MWANAFUNZI MIMBA NI KUMHARIBIA MAISHA
No comments:
Post a Comment