Sunday, April 15, 2012

Kili Awards 2012 events.......

DIAMOND ALIJINYAKULIA TUZO TATU KWA MPIGO......
Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora Kilimanjaro Music Awards 2012

“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa hivi, alisema Diamond baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.
Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo
 
                                                     Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake mara baada ya kupokea tuzo yake ya utunzi bora wa nyimbo.
 
Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo usiku huu.
 
Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda tuzo ya mburudishaji bora, wa pili kutoka kushoto ni mume wake na wengine ni watoto wake.
 
Kulia ni Msanii Profesa Jay na kushoto ni Mkubwa Fella meneja wa kundi la TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop.
 
Hapa Dyna akimvuta mtu kwake.......
Recho nae hakua nyuma..........
 
  Diamond katikati akiwa jukwaani na wenzake kabla ya kuimba wimbo wa msondo katika hafla ya kukabidhi tuzo za wanamuzikii bora za Kilimanjaro Music Award zainazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kulia ni Khalid Chokoraa wa bendi ya mapacha watatu na Ommy Dimpoz pale kati.......
 

Msanii HBaba akiwa amezungukwa na vimwana katika hafla hiyo

Mtayarishaji wa muziki P. Funk kulia akiwa na msanii wa muziki wa Hiphop Jay Moo.
 
Kulia ni Dina Marios wa Clouds akiwa na Asma Makau kutoka Clouds pia.
 
Mwanamuziki Ali Kiba akitoa shukuranbi zake kwa mashabiki wa muziki mara baada ya kutangazwa mshindi katika tuzo za muziki za Kilimanjaro Music Award zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo ameshinda kwa wimbo wake unaoitwa Dushelele
Mwmnamuzki Ali Kiba akipokea tuzo yake kutoka kwa Mtangazaji wa Clouds Dina Marios mara baada ya kutangazwa mmoja wa washindi katika tuzo hizo, kushoto ni mtangazaji wa ITV na Radio One Rainfredy Masako
Kundi la THT likitumbuiza katika tuzo hozo usiku huu.
 
Mchekeshaji Steve Nyerere akiwa katika picha ya pamoja na Sinta mwigizaji wa zamani.
Kulia ni Taji Liundi na mbunifu wa mavazi Asia Idarous wa Khamsini.
Mdau Kelvin Twisa ndani ya nyumba pia.
Meneja wa kinywaji cha Redds Vicktoria Kimaro akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni wadau Benny Kisaka, Mabakila, Evance na Juma Pinto.
 
Mdau Nick Butty yupo ndani ya nyumba pia.


No comments:

Post a Comment